Loading...
 

Uundaji wa Klabu- Kuunda Timu Ya Uanzilishi

 

Wasiliana na wanachama watazamiwa

 

Wasiliana na watu ambao wanaweza wakawa na nia ya kuwa wanachama wa klabu au ambao wanaweza kukusaidia nayo. 

Angalau wanachama 8 wanahitajika ili kuunda klabu mpya, lakini ni vizuri zaidi kama una wanachama kati ya 10 na 15 ili kuwa na klabu imara. Kama tayari unao wanachama watazamiwa, safi sana! Ruka kwenda hatua ya 7. Hamna haja ya wanachama waanzilishi kuwa wanachama wapya wa Agora. Inawezekana sana wanachama wote wapya wa klabu mpya kuwa wanachama wa klabu zingine:

 

Membership

 

Baadhi ya mawazo ya jinsi ya kuwaandikisha watu:

  • Weka kwenye akaunti zako za mitandao ya kijamii kuhusu nia yako ya kuanzisha klabu ya Agora Speakers na taarifa kuhusu Agora ni nini na ni kitu gani klabu itafanya.
  • Watumie barua pepe watu ambao una mawasiliano nao kuhusu mpango wako.
  • Watumie barua pepe rafiki au wanachama wa mashirika mengine yanayofanana ambao wanaweza kupendezwa na klabu.
  • Sambaza neno kuhusu Agora Speakers kuhusu mikutano unayoenda; waalike wanaohudhuria kwenye mkutano wa uanzilishi.
  • Sambaza neno kuhusu Agora kwenye makundi ya mitandao ya kijamii ambayo upo. Kama kundi linasimamiwa au linathibitiwa, inapendekezwa kuwa ufuate maoni ya watu waliopo, alafu watambue ambao wanaweza wakapenda mpango wako na toa maoni kwenye kundi kuwa umewatumia ujumbe binafsi, wataje majina ili kupata umakini wao. Endelea kuwasiliano nao kibinafsi.
  • Ongea na wanachama wa mashirika mengine ambao hawajaongeza muda wa uanachama wao.
  • Weka tukio kwenye tovuti kama Meet Up au Internations
  • Tangaza nia yako ya kuanzisha klabu kwenye aidha kundi la Facebook la Agora la nchini kwenu au - kama halijaundwa bado - kwenye kundi la Agora Speakers International.
  • Unda Google AdWords au kampeni Facebook ukilenga wanaotafuta "kujifunza kuzungumza mbele ya hadhira", "mazoezi ya uzungumzaji mbele ya hadhira", "kuogopa kuzungumza mbele ya hadhira," au viambatanisho vinavyofanana, weka vizuizi vya kijiografia vilivyo mathubuti (inafaa, mjini kwako)
  • Acha vipeperushi kwenye vyuo vikuu, maduka ya vitabu, maktaba, nk.
  • Google (Tafuta) blogsu, tovuti, baraza, na makundi kwenye eneo lako yanayohusu uzungumzaji wa mbele ya hadhira na uongozi, na weka ujumbe hapo. Jaribu kuepuka kuitwa barua taka (kuweka ujumbe mwingi), weka dhahiri kuwa Agora Speakers ni shirika lisilo la faida, na ada ni ndogo kabisa. 
  • Chapisha tangazo la bure kwenye gazeti au jarida la tamaduni la kiambo.
  • Andika na tuma taarifa kwenye magazeti au stesheni za redio.

 

Kupata mawazo zaidi, Google (tafuta) majina ya klabu ya mashirika mengine kwenye eneo lako, na uone sehemu ambazo wamejitangaza, alafu tumia njia hizo. 

Kuelezea Agora ni nini

Utakapokuwa unajaribu kuwasajili wanachama, unahitaji kujua jinsi ya kuelezea Agora inahusu nini.

NI wazo zuri kupitia taarifa zote na uwasilishaji uliopo kuhusu shirika letu ili uweze kuambatanisha nyaraka zinazofaa kwenye mawasiliano wako na uonyeshe faida kuu za kujiunga na klabu ya Agora Speakers. Ina manufaa kuonyesha uwasilishi huu mfupi.

Unaweza ukatumia maelezo haya ya dakika moja kuelezea Agora.

Kufuatilia waliovutiwa

Pale barua pepe na ujumbe kutoka watu wanaovutiwa vikianza kuingia, endelea kuelezea kazi za Agora na jinsi klabu inafanya kazi, na jinsi wanachama wa Agora wanavyofaidika.

Unaweza kutumia nyenzo rasmi ya Agora, aidha kama zilivyo au zilizobadilishwa kulingana na mahitaji yako. Unazipata kwenye wovuti wa chapa kwenye sehemu ya "Uwasilishi".

 

Kuandikisha Mwanachama

 

Wanachama wote wa klabu wanahitaji kujiandikisha kama watumiaji wa Jukwaa la Mtandaoni wa Agora ili kupita ufikivu wa mifumo ya Agora, ikiwemo nyenzo za kielimu. Waelekeze kwenye kiunganishi hiki ili waweze kujiandikisha.


Contributors to this page: agora and zahra.ak .
Page last modified on Monday August 30, 2021 01:43:39 CEST by agora.